Mourinho: Man City watakuwa hatari bila Sergio Aguero

Football
Typography

Mshambuliaji huyo wa Argentina, 28, amepigwa marufuku kucheza mechi tatu baada ya kumgonga mchezaji wa West Ham kwa kiwiko cha mkono mechi ambayo City walishinda 3-1.

Aguero amefunga mabao matatu katika mechi tatu alizocheza Ligi ya Premia msimu huu lakini Mourinho anasema kutokuwepo kwake kuna maana kwamba City, chini ya Pep Guardiola hawataweza kutabirika.

"Akiwa hachezi, basi wana wachezaji wengine wengi wanaweza kutumia," amesema Mourinho.

"Inakuwa vigumu zaidi. Sergio Aguero akiwepo basi unajua atacheza, na unajua watajipanga vipi."

Mourinho amesema mmoja kati ya Kelechi Iheanacho, Raheem Sterling na David Silva anaweza kuchezeshwa kama 'nambari tisa bandia' kwenye debi hiyo Old Trafford.

Source: BBC