Messi kuuguza jeraha wiki 3

Football
Typography

Timu ya Barcelona kutoka Uhispania itakosa huduma ya mshambuliaji wake matata Lionel Messi kwa kipindi cha wiki 3.

Timu ya Barcelona kutoka Uhispania itakosa huduma ya mshambuliaji wake matata Lionel Messi kwa kipindi cha wiki 3.

Messi alipata jeraha la mchanuko wa misuli hapo jana wakati wa mechi iliyochezwa kati ya Barcelona na Atletico Madrid.

Nyota huyo wa Argentina alishindwa kumalizia mechi hiyo na kulazimika kumwachia Arda Turan nafasi yake katika dakika ya 59 baada ya kupata jeraha.

Baada ya ukaguzi wa kiafya kufanyika, Barcelona imetoa maelezo na kubainisha kwamba Messi atauguza jeraha kwa kipindi cha wiki 3.