Messi ainusuru Albiceleste, Argentina 3-0 Colombia

Football
Typography

Ushindi wa mechi hio ilochezwa ugani Estadio San Juan del Bicentenario, San Juan, Argentina, umerudisha matumaini makubwa kwa Albicelestes baada msururu wa matokeo mabaya hivi karibuni katika mechi za kufuzu kwa Russia 2018.

Messi alifunga bao la kwanza mnamo wa dakika ya 10' na baadae kusaidia wenziwe kufunga mabao mengine mawili, Lucas Pratto (23') na Di Maria (84').

Argentina sasa ipo katika nafasi ya tano katika jedwali la America kusini na itanarajiwa vikubwa kutoshindwa kufuzu kwa dimba la dunia 2018.