Arsenal waanza vibaya raundi ya 16 bora

Football
Typography

Kwenye mechi hiyo iliyogaragazwa katika uga wa Allianza Arena nchini ujerumani wenyeji Bayern walikuwa wa kwanza kucheka na wavu kupitia kwa Arjen Robben kunako dakika ya 11 kabla ya Alexis Sanchez kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti na kuhakikisha kipindi cha kwanza kinakamilika sare.

Baada ya kuumia kwa mlinzi wake raia wa ufaransa Laurent Konscienly kunako dakika ya 49 na kufanyiwa mabadiliko na Gabriel Paulista Arsenal walivuja na kukubali mabao manne ya haraka yaliopachikwa na Robert Lewandowski kabla ya Thiago Alcantara kupachika mawili na kisha Thomas Muller kufunga hesabu hiyo ya mabao matano.

Sasa Arsenal watakuwa na kibarua cha kuwalaza Bayern kwa mabao manne kwa nunge kwenye mkondo wa pili nyumbani kwake emirates ili kufuzu kwa awamu ya robo fainali.

Wawakilishi hao wa uingereza iwapo watayaaga michuano hiyo watakuwa wanayaaga kwa msimu wa sita mfululizo kwenye awamu hiyo ya 16 bora.