FKF tawi la Mombasa kuwatuza mabingwa wa 2016

Football
Typography

Hafla hiyo itaandaliwa hapo kesho katika mkahawa wa Panaroma ulioko karibu na uwanja wa kaunti ya Mombasa kuanzia saa 6.30 jioni na kuongozwa na gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho pamoja na aliyekuwa waziri wa michezo katika serikali ya kaunti ya Mombasa Mohammed Abbas.

Kulingana na mwenyekiti wa FKF tawi dogo la Mombasa Goshi Juma Ally ni kwamba kila timu iliyoshiriki michuano hiyo itakabidhiwa sare na mipira miwili huku bingwa akijitilia kibindoni shilingi laki tano pesa taslim mshindi wa pili shilingi laki mbili unusu na kisha mshindi wa tatu akijiondokea na shilingi laki moja.

Itakumbukwa kuwa klabu ya Wananyuki FC kutoka mtaa wa Mwembe kuku ndio walioibuka mabingwa wa msimu huo baada ya kumaliza ligi wakiwa na alama 67 alama tatu zaidi ya Bamburi united huku LYSA na Goodhope wakimaliza kwenye nafasi za tatu nan ne mtawalia.