Changamwe United wajizoleya alama tatu za bure

Football
Typography

Kikosi cha Chamgamwe chini ya ukufunzi wake Jones Kyallo walipewa ushindi wa bure wa alama tatu na mabao mawili baada ya wapinzani wao KenGen Olkarai kushindwa kufika hapa Mombasa kwa ajili ya mchuano wa raundi ya pili.

Ushindi huo umewapa matumaini ya kufanya vyema baada ya kuweza kutoka sare ya kutofungana na Mwatate United kwenye mechi yake ya kwanza ugenini.

Kulingana na jedwali la ligi hiyo Changamwe wanaorodheshwa kwenye nafasi ya tatu wakiwa na alama nne sawa na VegPro wanaoshikilia nafasi ya pili huku Green berets wakiongoza na alama sita.

Mechi inayofuata watachuwana na Commercial FC kutoka Thika katika uga wake wa nyumbani wa Changamwe Estare Jumapili ya Aprili 9.