Wenger kutangaza msimamo wake karibuni

Football
Typography

Raia huyo wa ufaransa mwenye umri wa miaka 67 anakamilisha mkataba wake na arsenal mwishoni mwa msimu huu huku mustakabali wake ukiwa haujulikana na mashabiki wakishinikiza kuondoka kwake.

Wenger ameeleza kuwa anaendeleya na kazi yake na kuwa maneno ya kejeli kutoka kwa mashabiki hayamtatizi kwenye majukumu ya kuinowa klabu hiyo.

Kulingana na katibu mkuu wa klabu hiyo Ivan Gazidis aliwaambia mashabiki mwishoni mwa wiki kuwa mustakabali wa mkufunzi huyo anasalia na bodi ya klabu ambayo itatowa uwamuzi wake karibuni.

Arsenal walilazimishwa sare ya mbili mbili na Man city mwishoni mwa wiki na hapo kesho wanatarajiwa kuchuwana dhidi ya West ham kwenye mechi ya ligi kuu nchini uingereza.