Chipukizi wa Pwani wafanya vyema kwenye michuano ya kitaifa

Football
Typography

Mshambuliaji Khamis Nyale aliweza kuifungia pwani mabao mawili na kuulaza ukanda wa Magharibi kwa mabao mawili kwa nunge na kunyakuwa tuzo la mfungaji bora kwa kucheka na wavu mara tano kwenye michuano hiyo ya siku mbili.

Kwenye mechi za makundi vijana hao walitoka sare ya moja moja na ukanda wa magharibi kabla ya kuwalaza ukanda wa kati kwa mabao mawili kwa moja na kufuzu kwenye nusu fainali waliolazwa na Nyanza kwa mabao mawili kwa moja. 

Nairobi ndio walionyakuwa ubingwa huo baada ya kuwalaza Nyanza kwa mabao matano kwa manne kupitia matuta ya penalti baada ya kutoka sare ya kutofungana kwenye mda wa kawaida.

Wachezaji wanne kutoka kikosi hicho cha pwani Ibrahim Mone, Suleiman Juma, Roby Mangi na Khamis Nyale wameteuliwa kwenye kikosi cha vijana 34 watakaounda timu ya taifa kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 13 huku wakufunzi wao 

Patrick Nyale, Andrew Hadari Musungu alias Ada na Billy Mwangemi wakiteuliwa kama wakufunzi bora wa michuano hiyo.