Bandari Youth wainyeshea Crossroads mvua ya mabao kumi kwa moja

Football
Typography

Kwenye mechi iliyogaragazwa katika uga wake wa Mbaraki Chipukizi hao wa mkufunzi Swaleh Sunda walionyesha ari ya ushindi tangu mwanzo mwa mechi hiyo ambapo Twalib Hassan alicheka na wavu mara tano, Omar Matano akipachika mabao mawili kabla ya Jude Otieno,Washee Alphonce na Nassib Mwaruwa wakipachika bao moja kila mmoja wao.

Kwenye mechi nyengine za ligi hiyo zilizogaragazwa hapo jana:-

Omax 2 vs Desert FC 0

Ambassadors 2 vs LYSA 0

Good Hope 2 vs Bamburi FC 0

Annex 0 vs Magongo Rang 1

Mantubila 5 vs Eleven Stars 1

Wananyuki 1 vs Bodo Glimt 0

Umba 2 vs Soweto 0

Miritini 3 Vs 2 Wanderers