Chelsea wanyakuwa ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza

Football
Typography

Hii ni baada ya kuwalaza West Bromwich albion kwa bao moja kwa nunge usiku wa jana.

Bao hilo la pekee kwa vijana hao wa The Blues lilipachikwa wavuni na Michy Batshuayi zikiwa zimesalia dakika nane kabla ya kukamilika kwa mechi hiyo.

Huu ni ubingwa wa mara ya tano wa EPL kwa Chelsea.

Tottenham ambao ndio waliokuwa wapinzani wa karibu wa Chelsea katika nafasi ya pili, walipoteza mchezo wao dhidi ya West Ham Mei 5, na hivyo kuifanya Chelsea kuhitaji kushinda mechi mbili kati ya nne zilizosalia.

Antonio Conte amekuwa mkufunzi wan ne kunyakuwa ubingwa wa ligi hiyo kwenye msimu wake wa kwanza baada ya Jose Mouringo, Carlo Ancelloti na Manuel Pellegrini.