FKF yaweka sahihi mkataba na Mafro kwa sare za timu za taifa

Football
Typography

Hii ni baada ya kutia sahihi mkataba wa shilingi milioni 75 kwa mwaka ambapo shirika hilo litatoa sare 600 kwa timu zote za timu za taifa.

Mkataba huo utapelekeya shirikisho la FKF kupokea hela kwa timu za taifa kuvalia sare zenye chapa ya shirika hilo la nchini Ghana.

Harambee stars watavalia sare rangi nyekundu kwenye mechi zake za nyumbani huku za rangi ya kijani kwa mechi za ugenini na sare nyeupe za dharura huku wakitarajiwa kuanza kuvaa sare hizo mwezi juni ambapo watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Angola huku timu ya taifa kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 13 wakivaa nchini uingereza wakichuwana na Southampton.

Timu nyengine za taifa zenye kuvalia sare za shirika hilo ni timu za taifa za Zimbabwe na Zambia pamoja na klabu za Nkana na Power Dynamos za Zambia.