Agege ajiunga rasmi na Sporting ya nchini Ureno

Football
Typography

Mchezaji kinda wa Kenya anayesakata soka ya kulipwa nchini Qatar Mohamed Katana almaarufu Messi amejiunga rasmi na klabu ya Sporting Lisbon ya nchini Ureno kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mchezaji kinda wa Kenya anayesakata soka ya kulipwa nchini Qatar Mohamed Katana almaarufu Messi amejiunga rasmi na klabu ya Sporting Lisbon ya nchini Ureno kwa mkataba wa miaka mitatu.

Agege ambaye amekuwa akichezeya klabu ya Aspire nchini Qatar amewahi kugonga vichwa vya habari mara kwa mara na kutia fora mwezi Februari mwaka jana alipoisaidia klabu yake hiyo ya awali kunyakuwa michuano ya kimataifa ya Al Kass ambapo alipachika mabao manne mawili dhidi ya chipukizi wa Real Madrid na mengine dhidi ya inter Milan na Benfica.

Messi aliwahi kuchezeya klabu za Goodhope na Black star katika eneo la Kisauni kabla ya nyota yake kungara na kujiunga na Aspire baada ya majaribio yaliofanywa katika uga wa Kasarani jijini Nairobi.

Mapema mwaka huu pia aliwahi kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Kenya kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 20 ambapo walishiriki kwenye mechi dhidi ya Senegal.

Vilevile amepuuziliya mbali madai kuwa amekuwa kwenye majaribio na klabu ya nchini Uswidi na kusema kuwa alikuwa nchini humo kwa likizo kabla ya kuelekeya nchini Ureno ambapo amekamilisha uhamisho rasmi.