Kisauni watinga nusu fainali Ngano Cup

Football
Typography

Kwenye robo fainali ya kwanza iliyogaragazwa katika uga wa Mombasa Sports Club bao la Idha Amin kunako dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza lilitosha kuwahakikishia kisauni nafasi kwenye nusu fainali ya michuano hiyo.

Kwenye awamu ya makundi Kisauni walimaliza kileleni mwa kundi A wakiwa na alama nne baada ya kushinda mechi moja kupoteza moja na kutoka sare moja.

Leo hii robo fainali ya pili itagaragazwa katika uga uo huo kati ya Mtongwe dhidi ya Somali youth kuanzia majira ya saa kumi kamili alasiri.

Hii ni awamu ya kumi na moja ya michuano hii mikubwa hapa Mombasa na ukanda mzima wa Pwani ambayo huandaliwa kila mwaka na kampuni ya Mombasa maize millers kwa ajili ya kukuza vipaji na pia kuburudisha wapenzi wa soka.