Coast Stima wanusa Supa ligi

Football
Typography

Kwenye mechi ya ligi ya daraja la kwanza iliyogaragazwa katika uga wa Wundanyi kaunti ya Taita Taveta Bakari Ojiambo alipachika mabao mawili kupitia mikwaju ya frikiki huku Nicholas Kanyakle akikamilisha hesabu hiyo.

Kwenye mkondo wa kwanza katika uga wa Kabete jijini Nairobi Kangemi walipata ushindi mwembamba wa bao moja kwa nunge.

Kutokana na kupoteza kwa mechi hiyo Coast stima wamekwea kileleni mwa jedwali wakiwa na alama 44 baada ya kushiriki mechi 20 huku mechi nne pekee zikisalia kukamilika kwa ligi hiyo.

Kangemi ni wa pili alama moja nyuma ya stima na kisha Mwatate ni watatu wakiwa na alama 34 wakishiriki mechi 19.