Rahma Fc yalazwa 4-2 na Humberg Fc

Football
Typography

Mecho hiyo iliyosakatwa katika uwanja wa Mbuzi Kongowea hii leo jioni ilivutia halaiki ya watazamaji ambao wengi wao ni mashabaiki wa idhaa ya Rahma.

Licha ya Rahma Fc Kuonyesha mchezo mzuri  katika mechi hiyo walionekana kushindwa nguvu na wenzao wa Hamburg ambao wana uzoefu wa siku nyingi na hivyo kuwalaza Rahma Fc kwa mara ya kwanza tangu timu hizo mbili kukutana.

Mabao ya Hamburg Fc yalitiwa wavuni na Moroso, Yaba Bobo, Jacaranda na Maulidi almaaruf Paulo maldini.

Mabao ya Rahma Fc yalifungwa na Hussein na Ibrahim Meja .

Baada ya mechi hiyo naodha wa Hamburg Omar Batistuta ameipongeza Rahma Fc Kwa kuonyesha mchezo mzuri na kuwataka kuendelea kukifua kikosi chao ili kuweza kuandikisha matokeo mazuri siku za mbeleni.

Kwa upande wake nahodha wa Rahma Fc Luqman mahamoud ametaja ukosefu wa zoezi kama sababu kuu ya kufungwa kwa kikosi chake.