25
Sun, Feb

Spurs na Wanyama watinga raundi ya 5 FA

Football
Typography

Wanyama na Spurs waliandikisha ushindi wa mabao mawili kwa nunge katika mechi ya marudiano ugani Wembley, London, Jumatano usiku.

Mabao hayo yakipachikwa na Butler (bao la kujifunga mwenyewe) na Lamela mnamo dakika ya 26' na 34' mtawalia.

Itakumbukwa kua mkondo wa kwanza wa raundi ya nne ulilazimisha marudiano ya mechi hio baada ya Harry Kane kusawazisha natija kua 1-1 kusini Wales, katika uga wa Rodney Parade.

Meneja wa Spurs Pochettino amesisitiza umuhimu wa timu yake kujizatiti kunyakua kombe la Emirates FA huku akionekana kukata tamaa ya taji la Ligi 2017/18 kutokana na tofauti kuu dhidi yao na Manchester City.

Sasa katika mechi ya kwanza ya raundi ya tano ya komble la FA, Spurs watacheza dhidi ya Rochdale A.F.C. Jumapili 18, Februari 2018.