25
Sun, Feb

Copa Del Rey - Marudio ya mechi ya Valencia na Barca

Football
Typography

Alhamisi hii ndio marudio ya mechi hiyo iliomalizika kwa ushindi wa Barca 1-0 wiki ilopita Nou Camp.

Ni miaka 10 tangu Valencia kufika finali ya dimba hilo na msururu wa matokeo mema msimu huu utawapa matumaini makubwa jioni ya leo dhidi ya Blaugrana.

Katika mechi ya kwanza ya nusu fainali hio wiki iliopita, nyota wa Uruguay Luis Suárez alifungia Barca bao la pekee mnamo dakika ya 67'.

Aidha kufuatia jeraha dogo la Pique wikendi jana, huenda Yeri Mina aliesajiliwa hivi majuzi akapata nafasi ya kucheza mechi yake ya kwanza ugenini Mestalla.