25
Sun, Feb

Barcelona kuvaana na Sevilla fainali ya Copa Del Ray baada kuwalaza Valencia.

Football
Typography

Mshambuliaji Philiphe Coutinho amefungua akaunti yake ya mabao na klabu yake mpya ya Barcelon baada ya kufunga bao la kwanza na kuisaidia kutinga fainali za Copa Del Ray.

Raia huyo wa Brazili alipachika bao kunako dakika ya 49 huku Ivan Rakitic akifunga mchezo kwa bao la pili zikiwa zimesalia dakika nane kukamilika kwa mchezo huo wa nusu fainali ya pili mkondo wa pili.

Barca walikuwa wameshinda kwa bao moja kwa nunge kwenye mkondo wa kwanza nyumbani Camp Nou.

Sasa miamba hao wa Uhispania watavaana na Sevilla ambao waliwabandua nje Leganes kwenye nusu fainali ya kwanza ya dimba hilo.

Fainali hiyo inatarajiwa kugaragazwa Aprili 21 mwaka huu.

Barca wamenyakuwa taji hilo kwa miaka mitatu mfululizo na watakuwa wanalenga kuendeleza historia ya kunyakuwa kwa mwaka wan ne.