25
Sun, Feb

Gor na AFC kuanza kampeni za barani Afrika

Football
Typography

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu nchini Gor mahia kuanza kampeni zake za ligi ya klabu bingwa barani Afrika pale watakapoivaa Leones Vegetarianos ya Equatorial Guinea kwenye mechi ya muondoano.

Gor watashuka ugani Kenyatta kaunti ya Machakos mchana wa leo kusaka tiketi ya kufuzu kwa raundi ya pili na awamu za makundi mtawalia.

Kulingana na mkufunzi wa Gor Dylen Kerr kikosi chake kiko imara kuweza kujizolea alama tatu muhimu na kuhakikisha klabu hiyo inarudi kwenye enzi zake za kutamba kote barani Afrika.

Kwa upande wao AFC Leopards watakuwa wanapeperusha bendera ya Kenya kwenye michuano ya shirikisho barani Afrika hapo kesho pale watakapoialika Fosa Juniors ya Madagascar ugani Bukhungu kaunti ya Kakamega.

Klabu hizo mbili zinatarajiwa kucheza mechi zake za ligi kuu katikati ya wiki.