25
Sun, Feb

Agüero aiadhibu Leicester City

Football
Typography

City waendeleza matokeo mazuri katika EPL baada ushindi huo mnono dhidi ya Leicester.

Sterling alifunga bao la kwanza mapema mnamo dakika ya 3' huku 'Foxes' wakisawazisha kupitia Vardy dakika ya 24'. Mechi hio ikielekea muda wa mapumzika ikiwa sare ya 1-1.

Kipindi cha pili kilishuhudia mabao yaliosalia kufungwa na nyota Agüero dakika za 48', 53', 77' na 90'.

ManCity sasa wako alama 16 juu ya mahasimu wao Manchester United. Ligi hio inatarajiwa pakubwa kukamilika na ManCity wakiwa mabingwa msimu huu.

Hapo Jumanne, City watasafiri Uswizi kucheza mechi ya kwanza raundi ya 16 katika ligi ya mabingwa bara Ulaya dhidi ya FC Basel.