25
Sun, Feb

Ronaldo atoa onyo kali kwa Neymar na PSG

Football
Typography

CR7 aonesha umahiri wake dhidi ya Real Sociedad kwa kufunga hatriki usiku wa Jumamosi, Je hili ni onyo kwa PSG?

Fomu hio ya Los Blancos imekuja wakati muafaka kwani mabingwa wa Ufaransa PSG wanatarajiwa ugani Bernabeu Jumatano (Feb 14) kwa mechi ya kwanza (raundi ya timu 16) katika Ligi ya mabingwa bara Ulaya, UEFA-CL.

Hatriki hio ya Ronaldo ndio yakwanza msimu huu, huku mechi hiyo ikimalizika Real Madrid 5 - 2 Real Sociedad.

Neymar na PSG wameitaja mechi hiyo ya Jumanne kua muhimu zaidi msimu huu na wameahidi kujikakamua mia fil mia Bernabeu.

Neymar alifunga bao la pekee katika mechi ya Ligi kuu Ufaransa dhidi ya Toulouse Jumamosi.

Itasalia kuonekana kama Madrid watabadili msururu mbaya katika LaLiga na kusonga mbele katika ligi ya mabingwa bara Ulaya ambayo wengi wameitilia upato kufuzu kwa robo fainali. 

Zidane anakizungumkuti cha kuamua iwapo BBC (Bale, Benzema na Critiano) watarejea kuanza mechi hiyo ya Jumatano pamoja.