25
Sun, Feb

Coast Stima waanza na sare NSL huku Modern wakilazwa

Football
Typography

Wageni Coast Stima waliwalazimisha wenyeji wao Green Commandoes sare ya moja moja ugenini kwenye mechi yake ya kwanza kwenye michuano ya supa ligi.

Kwenye mechi iliyogaragazwa ugani Bukhungu kaunti ya Kakamega Commandoes walikuwa wa kwanza kucheka na wavu kunako dakika za mwanzo za kipindi cha pili kupitia kwa Henry Atola lakini Collins Kombo akaihakikishia alama moja Stima zikiwa zimesalia dakika tano kukamilika kwa mchezo huo.

Sare hiyo inawaweka wawili hao kwenye nafasi za nane wakiwa na alama moja.

Mkufunzi wa Green Commandoes Brenden Mwinamo amelalamikia bao rahisi walilofungwa akisema ni hali ya mchezo na kuwa watarudi kujipanga kwa ajili ya mchezo wa pili.

Coast Stima wanatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kisumu Allstars siku ya Jumamosi ugani Mbaraki huku Modern waliolazwa na Western Stima kwenye mchezo wa kwanza kwa mabao mawili kwa nunge watakuwa mwenyeji wa KCB.