25
Sun, Feb

Awamu ya 16 bora UEFA kuanza leo

Football
Typography

Klabu mbili za uingereza zitashuka ugani usiku wa leo kuanza kampeni za kujitaftia tiketi za robo fainali za michuano ya klabu bingwa barani ulaya UEFA.

Hii ni pale awamu ya 16 bora itakapoanza leo baada ya mapumziko marefu.

Vinara wa ligi kuu nchini uingereza Manchester city watakuwa ugenini kuvaana na Basel huku wenzao Totenham Hotspurs pia wakisafiri nchini Italia ambapo watachuwana na Juventus.

Mechi zote mbili zitaanza saa tano kasorobo usiku wa leo.

Hapo kesho itakuwa zamu ya vijana wa Jurgen Kloop Liverpool watakaovaana na FC Porto huku PSG wakiivaa Real Madrid.