25
Sun, Feb

Chelsea wajizolea alama tatu dhidi ya Westbrom

Football
Typography

Vijana wa Atonio Conte Chelsea wamejikakamua na kujipatia suhindi wa mabao matatu kwa nunge dhidi ya West Bromwich Albion.

Kwenye mechi ya pekee ya ligi kuu nchini Uingereza iliyochezwa usiku wa jana raia wa Ubelgiji Eden Hazard alipachika mabao mawili kunako dakika za 25 na 71 huku Victor Moses akifunga moja dakika ya 63.

Alama tatu hizo muhimu zimewapaisha Chelsea hadi nafasi ya nne kwenye jedwali wakiwa na alama 53 alama moja nyuma ya Liverpool na alama moja zaidi ya Tottenham walioko kwenye nafasi ya tano.

Kwa upande wao West Brom wanaendelea kudidimia mkiani wakiwa na alama 20 baada ya kushiriki michezo 27.

Kibarua cha Chelsea kinachofuata kwenye ligi kuu kitakuwa dhidi ya mashetani wekundu wa Manchester United Februari 25.