Bandari waendeleza msururu wa kutopoteza mechi hata moja

Spoti
Typography

Wawakilishi wa pekee wa Pwani kwenye ligi kuu Bandari FC wameendeleza matokeo mazuri kwenye ligi kuu baada ya kuwalaza wageni Muhoroni youth kwa mabao matatu kwa  nunge.

Wawakilishi wa pekee wa Pwani kwenye ligi kuu Bandari FC wameendeleza matokeo mazuri kwenye ligi kuu baada ya kuwalaza wageni Muhoroni youth kwa mabao matatu kwa  nunge.

Kwenye mechi iliyogaragazwa ugani Mbaraki hapa Mombasa Bandari walijipati mabao yake hayo kupitia raia wa Uganda Dan Sserenkuma kunako dakika ya 30 kabla ya Shaban Kenga na Mussa Mudde kuongeza la pili na la tatu mtawalia.

Kulingana na mkufunzi wake Paul Nkata amesema kuwa matokeo hayo mazuri yanatokana na safu yake ya ulinzi ambayo haijakubali bao hata moja huku akisema kuwa wanachukulia kila mechi kama fainali.

Kwa sasa Bandari ambao wameshinda mechi mbili na kutoka sare moja wanaongoza jedwali na alama saba na watachuwana dhidi ya Ulinzi kwenye mechi inayofuata ugani Afraha kaunti ya Nakuru.