22
Thu, Feb

Kaya Tiwi wahifadhi ubingwa kwenye michezo ya Shule

Spoti
Typography

Vijana hao wa mkufunzi Philip Onyango walionyesha ari yake tangu kwenye mechi ya makundi hadi kunyakuwa ubingwa huo huku mchezaji wake Maria Komba akiteuliwa kama mchezaji bora kwenye mpira wa vikapu kwa wanawake.

Laiser Hill kutoka bonde la ufa wameibuka mabingwa wa mpira wa vikapu kwa wanaume baada ya kuwalaza Upper hill, St. Cecilia Misikhu ikanyakuwa ubingwa wa mpira wa magongo kwa wanawake, nao St. Anthony Kitale ikanyakuwa kwa wanaume.

Kwa ujumla ukanda wa bonde la ufa wamemaliza kidedea kwa alama 82, Nairobi wakiwafata kwa alama 60 pwani wamemaliza kwenye nafasi ya sita kwa alama 35.