Barca waongeza ada ya kumsajili Coutinho hadi €160M

Spoti
Typography

Philippe Coutinho anazidi kukaribia kuwa mchezaje wa Barcelona baada ya Klabu hi ya Catalonia kuongeza kiwango cha pesa kumsajili nyota huyo wa Brazil.

Kulingana na gazeti maarufu la Uhispania "MARCA", Barcelona sasa wameogeza ada hio hadi kufikia Euro milioni 160.

Iwapo watafaulu kumsajili Countinho, Barca watakua wamevunja rekodi ya Klabu hio ya kusajili mchezaji ghali zaidi.

Aidha Coutinho hatoweza kuchezea Barcelona katika ligi ya mabingwa ya bara Ulaya (UEFA CL) baada ya kuchezea Liverpool katika ligi hio msimu huu 2017/18.

Mazungumzo ya kukamilisha usajili huo yapo 'kileleni' kulingana na repoti kutoka Uhispania huku habari zingine zikidukuu kumalizika kwa dili hio mapema wiki ijayo.