Mwili wa afisa wa polisi wapatikana na majeraha kichwani Kibarani

Mwili wa afisa wa Polisi umepatikana umetupwa katika eneo la Kibarani hapa Mombasa. Akithibthisha kisa hicho kamanda wa polisi eneo bunge la Jomvu Lydia Wanjiru amesikitishwa na mauaji ya afisa wa...

Serikali ya kitaifa na kaunti zatakiwa kushirikiana kuwawezesha wavuvi kwa vifaa vya kisasa

Ipo haja ya serikali ya kitaifa na zile za kaunti kushirikiana kuhakikisha inawekeza zaidi kwa kuwawezesha wavuvi kupata vifaa kuvua katika bahari kuu.Gavana wa Lamu Issa Timamy ambaye pia ni...

Katibu Mkuu wa UDA Cleophas Malala sasa anasema chama hicho kinakusudia kusajili angalau wanachama milioni 15 ifikapo 2027.

Akizungumza siku ya Alhamisi, Malala alisema chama hicho kwa sasa kina wanachama milioni 9.98.

Aliwataka waratibu wa chama kulichukulia kwa uzito mkubwa zoezi la uandikishaji wanachama katika mikoa yao.

Malala alisema UDA lazima ishinde uchaguzi wowote kwa wingi wa kura kwa kuzingatia uzito wa uanachama wa chama.

Tangu kuwa katibu mkuu wa UDA, Malala amekuwa akishinikiza kusajili wanachama katika ngome za upinzani.

Alizungumza alipokuwa akimkaribisha naibu rais Rigathi Gachagua kwa mkutano na waratibu wa UDA katika makao makuu ya chama.

Gachagua alisema tayari, UDA imechukua maeneo ambayo Jubilee na ODM vilikuwa vyama maarufu zaidi na wimbi linaendelea kubadilika kwa upande wao.

 


RadioRahma ads