Hatimae Muungano wa mabaharia nchini SUK umeandaa uchaguzi wake rasmi katika ukumbi wa Licodep eneo bunge la Likoni kama ilivyoratibiwa baada ya uamuzi wa mahakama ya leba.
Katika uchaguzi huo, uliohusisha nafasi tatu za kupiganiwa, Mwalimu Chii Hamisi ameibuka mshindi katika nafasi ya mwenyekiti kwa kupata kura 110 huku mpinzani wake Khalfani Jillani Mwabonje akipata kura 57.
Atie Swaleh Ramadhan ndiye katibu mkuu wa muungano huo baada ya kupata kura 131 na kumshinda mpinzani wake Apollo Odhiambo Orao aliyepata kura 33.
Katika nafasi ya mweka hazina, John Hussein Zappa ameshinda kwa kupata kura 83 na kumshinda mpinzani wake wa karibu Suleiman Omar Boma aliyepata kura 76.
Aidha jumla ya watu 171 wameshiriki katika uchaguzi huo.
Kulingana na mwenyekiti wa bodi ya uchaguzi wa muungano huo Samson Menza, sasa viongozi hao wapya watakuwa na jukumu la kukuza chama hicho baada ya kukumbwa na mgogoro kwa zaidi ya miaka miwili.
Khalfani Jillani na mwenzake Suleiman Boma wamepongeza viongozi waliochaguliwa licha ya wao kushindwa, wakiahidi kuwapa ushirikiano kwa manufaa ya mabaharia wote kwa jumla.
Kwa upande wake Atie Swaleh ambaye ndio katibu mkuu ameahidi kuangazia masuala ya ajira ya mabaharia ambao kwa muda murefu wamesalia bila ajira pamoja na kuandikishwa upya kwa mabaharia.
Ikumbukwe kuwa uchaguzi huo unajiri baada ya mahakama ya leba kubatilisha uchaguzi wa awali wa mwaka 2021 kwa kutozingatia sheria ambapo mwezi Februari mwaka huu mahakama hiyo ilitoa uamuzi wa kuundwa kwa bodi ya uchaguzi na kuandaliwa kwa uchaguzi mpya.

Haya yanajiri huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya mabaharia Juni 25.

 


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo