Waziri wa Afya Susan Nakhumicha ameonya kwamba serikali inaweza kuwafuta kazi madaktari wanaogoma huku mzozo kati ya madaktari na wizara yake ukiendelea.

Madaktari wanaendeleza mgomo tangu juma lililopita wakilalamika kuwa serikali imeshindwa kuwaajiri wanafunzi waliohitimu mafunzo ya utabibu, kutofuata Mkataba wa Majadiliano ya Pamoja wa Madaktari wa 2017 (CBA) miongoni mwa masuala mengine.

Huku mgomo huo ukiingia siku yake ya nane hii leo, Nakhumicha anashikilia kuwa madaktari hao wanakiuka agizo la mahakama lililowaagiza kusitisha mgomo huo na wako katika hatari ya kupoteza kazi zao kwa kukosa kuripoti kazini.

Hadi kufikia wiki hii, chama cha madakatari KMPDU na serikali wamefanya mikutano miwili kuhusu suala hilo, lakini matokeo yaliyotarajiwa kutoka mikutano hiyo hayakuafikiwa.

Kufuatia mkutano wa Jumatatu, Nakhumicha alisema walikuwa wameafikiana na KMPDU kwamba Hazina ya Kitaifa ilikuwa imetoa mwanga wa kijani juu ya kuwaajiri wanafunzi waliohitimu mafunzo kuanzia Aprili 1.

Pia alitangaza kuwa wizara yake itaendelea na mazungumzo wiki hii na kwamba ada zote zinazosubiriwa kulingana na mkataba wa maelewano wa 2017 zitaidhinishwa kulingana na maagizo ya mahakama.

Hatahivyo Lakini maafisa wa KMPDU walipuuzilia mbali mazungumzo hayo, wakisema mgomo bado unaendelea


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo