Kinara wa ODM Raila Odinga amekanusha madai ya Naibu Rais William Ruto kwamba aliajiri wahuni ili kusababisha fujo katika mkutano wake Jacaranda, Nairobi, Jumapili.

Katika taarifa ya msemaji wake Dennis Onyango, Raila alisema Ruto ndiye aliyesababisha kutatiza kwa mkutano wake mwenyewe.
Kiongozi huyo wa ODM amesema ghasia za Jacaranda zilifadhiliwa na Ruto ili kuchochea vita katika eneo lake Bonde la Ufa ili kusababisha kufurushwa kwa wasio Wakalenji.

Raila alimlaumu Ruto kwa masaibu yake akisema, hata hivyo, watu walikuwa wakilipwa kuhudhuria mkutano wake wa Jacaranda na kwamba hiyo ilitosha kusababisha machafuko yaliyoshuhudiwa Jumapili.

Ruto wakati wa mkutano wake huko Jacaranda alimshutumu kiongozi huyo wa ODM kwa kuajiri vijana kupiga mawe mkutano wake na kusababisha vurugu.

Alimlaumu kwa kuwa na tabia ya kupanga kejeli na kurusha mawe mikutano yake ya kisiasa haswa katika maeneo ambayo anaungwa mkono sana.