Idara ya usalama kaunti ya Kwale imeanzisha oparesheni ya kuwasaka wanafunzi ambao hadi kufikia sasa hawajajiunga na kidato cha kwanza ili kutimiza agizo la serikali la asilimia 100.

Kwenye kikao na wanahabari ofisini mwake Kamishna wa kaunti ya Kwale Gedion Oyagi amesema kuwa oparesheni hio inahusisha machifu pia ili kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anayesalia nyumbai.

Wakati uo huo amewataka wazazi kujituma kutafutia watoto wao basari akisema kuwa hatua hio itasaidia kupunguza idadi ya watoto wanaosalia majumbani.

Ameeleza kuwa wanafunzi 94 wamepata ufadhili wa benki ya Equity kaunti ya Kwale huku akiwarai wazazi kutumia fursa hio kuwaelekeza vyema wanawao wanapokuwa majumbani ili kupata matokeo bora.

Haya yanajiri huku takwimu zikionyesha kuwa ni asilimia 90 ya wanafunzi kaunti ya Kwale wamejiunga na kidato cha kwanza wengi wakifadhiliwa na serikali ya kaunti.