Huku zikiwa zimesalia takribani siku 52 kufikia kwa kwa uchaguzi mkuu,wito umetolewa kwa wakaazi hapa Mombasa kuthibisha kama wamesajiliwa kama wapiga kura pamoja na kuthibitisha vituo vyao vya kupiga kura.

Akitoa wito huo mgombea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amesema kuna baadhi ya wapiga kura wengi walihamishwa kutoka kwenye vituo walivyosajiliwa hali ambayo amesema huenda ikatatiza zoezi la upigaji kura katika uchaguzi mkuu ujao.

Nassir amesema atafuatilia suala hilo kwa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapiga kura katika vituo walivyosajiliwa.

Huku hayo yakijiri Abdulswamad Shariff Nassir anapania kuweka miradi mbalimbali ya kiuchumi ili kuinua maisha ya wakaazi.

Akizungumza wakati akiendeleza kampeni zake eneo bunge la Jomvu Nassir,amesema ataweka miradi ya special Economic Zone eneo la Miritini na Dongokundu ili kuweza kufungua nafasi ajira kwa vijana wa kaunti ya Mombasa.

Kulingana na Nassir ni kuwa asilimia 47 ya vijana hapa Mombasa wanakumbwa na changamoto ya ajira.