Gavana mteule kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ameahidi kutatua lindi la ukosefu wa ajira linalowakumba vijana wa kaunti ya Mombasa.

Akizungumza katika kikao na bodi ya huduma ya utumishi wa umma katika ukumbi wa mafunzo ya kiserikali hapa mjini Mombasa Nassir amesema katika takwimu za mwisho kuhusu ukosefu wa nchini zilizotolewa na shirika la kuthatmini taqwimu nchini KEBS ziliashiria kuwa kaunti Mombasa asilimia 47 ya vijana hawana ajira.

Nassir amesema Agenda yake sasa ni kuhakikisha kuwa raslimali zinazopatikana ndani ya kaunti ya Mombasa zinawaa wakaazi.

Kulingana naye serikali ya kaunti ya Mombasa itakuwa chaguo bora kwa wakaazi wa Mombasa.

Nassir na naibu wake Francis Thoya wanatarajiwa kuapishwa siku ya Alhamisi wiki hii.