Huku Ulimwengu ukiadhimisha siku ya afya ya akili,imebainika kuwa Magonjwa ya akili yanazidi kuongezeka jijini Mombasa.

Kulingana na daktari wa magonjwa ya akili katika hospitali ya Portrz Nancy Kepkemboi magonjwa ya akili jijini Mombasa yanasabishwa na utumizi wa dawa za kulevya pamoja ,unyanyasaji wa kijinsia na migogoro ya kifamilia.

Akizungumza katika kituo cha kushughulikia wagonjwa wa akili cha Mombasa Women Hospitali eneo la Miritini,Nancy amewataka wazazi kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya kuchunguzwa akili,punde tu wanapohisi wasisi.

Wakati huo huo ameitaka jamii kutowatenga watu wenye matatizo ya akili,akisisitiza kuwa jamii inasahili kuwakubali watu wenye matatizo ya akili na kutowatenga.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kituo cha Women Empowerment and Rehabilitation Centre,Bi Amina Abdalla,ametaja kuwa kufikia sasa zaidi ya watu 300 wametibiwa na kupona matatizo ya akili katika kituo hicho.

Kwa sasa kituo hicho kina wagonjwa wenye matatizo ya akili 103 ambapo wanapokea matibabu pamoja na ushahuri nasaha na taaluma mbali mbali kama vile ususi na ufugaji.