Ukosefu wa wauguzi kujua jinsi ya kushughulikia majanga kuliwasababishia wao kuwa na wasiwasi wakati wa janga la Covid-19.

 Ruth Keah na taarifa zaidi.

Akizunguma na waandishi wa habari wanaoandika habari za Sayansi kwenye warsha iliyoandaliwa kwa njia ya mtandao na muungano wa wanahabari nchini wa MESHA, Anne Mweu kutoka kwa muungano wa wauguzi nchini alisema ilikuwa wakati mgumu hasa ikizingatiwa kuwa ilikuwa mara ya kwanza kwa baadhi ya wauguzi kushuhudia hali hiyo.

Kutokana na hali hiyo hata hivyo Bi Mweu alisema walilazimika kuwafunza wauguzi na hata wahudumu wengine wa afya ili kusaidia katika kushughulikia hali hiyo.

Alitoa wito kwa idara husika kuhakikisha kuwa wauguzi wanapewa hamasa za mara kwa mara ya jinsi ya kufanya kazi kwa mazingira yoyote yale iwe ni ya dharura ama la.

Usemi,ulioungwa mkono na Daktari Patrick Oyaro mkurugenzi mkuu wa shirika la USAID Stawisha Pwani.

Daktari Oyaro alisema miongoni mwa mikakati ambayo wanafanya ni kutoa hamasa kwa wauguzi na kujua ni vipi wanaweza tumia rasilimali walizo nazo kutoa huduma za afya kwa usawa.

Daktari Oyaro alisema japo shirika la afya ulimwenguni WHO lilisema covid-19 sio tena dharura ya kimataifa ya umma inayotia hofu, Daktari Oyaro amesema kuna haja ya jamii kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuzingatia kanuni za afya kila wakati.