Wadau mbalimbali wameonyesha wasiwasi wao wa jinsi chanjo ya Covid-19 inavyosambazwa katika bara la Afrika.

Katika hotuba yake ya kufungua kongamano la 8 la kanda kuhusiana na mbinu za kupunguza majanga- Disaster Risk Reduction lililoandaliwa jijini Nairobi, Mkuu wa kitengo hicho katika umoja wa mataifa Mami Mizutori amesema ni jambo la ksuikitisha kuona afrika imepokea idadi ndogo ya chanjo hadi sasa licha ya bara la Afrika kushinikiza uwepo wa sekta ya afya katika mkataba wa Sendai wa kupunguza majanga.
Amesema bara la Afrika limechangia pakubwa katika kufanikisha mkataba huo hasa katika uvumbuzi wa mbinu mbalimbali za kukabiliana na majanga ya kiafya ikiwemo kupambana na ugonjwa wa Ebola, Virusi vya HIV , Malaria miongoni mwa magonjwa mengine.
Hadi kufikia sasa, bara la Afrika limenakili zaidi ya visa milioni 7 vya virusi vya Corona huku karibu watu 175,000 wakipoteza maisha yao.
Huku kiwango cha watu waliopokea chanjo ya virusi vya corona katika bara la Afrika ikiwa asilimia 5 pekee.
Amesema kuna haja ya chanjo hizo kufikia jamii yote kwa usawa ili kuweka usawa wa afya kwa wote.


 

More Stories

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo