Mataifa barani Afrika yameshauriwa kuwekeza zaidi katika miradi ya kupunguza kutokea kwa majanga.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la 8 la kanda ya Afrika kuhusu upunguzaji wa hatari ya majanga,Mkurugenzi mkuu wa IGAD Climate Prediction and Application Centre (ICPAC) Daktari Guleid Artan amesema ili kupunguza majanga kutokea, kuna haja ya mataifa kuja na mbinu za kisasa ambazo zitaweza kutumika kwa urahisi na wananchi kuchukua tahadhari.

Daktari Guleid amesema mataifa yanafaa kuchukua swala la kupunguza majanga kama endelevu hasa ikizingatiwa majanga yanasababishwa na mabadiliko ya tabia nchi yanayoshuhudiwa kwa sasa.

Amesema kwa sasa bara hili la Afrika linakumbwa na kiangazi ambacho kimesababisha watu milioni 26 kukodolea tatizo la uhaba wa chakula.

Wito huo unakuja siku chache tu baada ya IGAD kufungua kituo ambacho kinatoa taarifa za mapema kuhusu hatari ya majanga jijini Nairobi.

Akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa umoja wa Afrika Mouse Mahamat, balozi Josefa Leonel Correia Sacko kutoka Angola amesema amefurahishwa na hatua ambazo zimechukuliwa na mataifa kadhaa kutekeleza maazimio ya mkataba wa Tunis ikiwemo kuunda mbinu mpya za kutoa taarifa mapema kuhusu hatari ya majanga.


 

More Stories

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo