Wito umetolewa kwa mataifa barani Afrika kujumuisha watu wenye ulemavu katika miradi ya kupunguza kutokea kwa majanga.

Hii ni kwasababu wakati majanga yanapotokea, watu wenye ulemavu huathirika kwa kiwango tofauti wanapokosa usaidizi.

Mfano hai ikiwa kutoka kwa Simon Munde kutoka nchini Malawi aliye mlemavu ambapo kulingana naye mwaka wa 2015 taifa la Malawi liliposhuhudia majanga katika wilaya 15 kati ya 28, watu wenye ulemavu waliathirika vibaya.

Hatua iliyosababisha taifa hilo kuwajumuisha watu wenye ulemavu katika miradi mbalimbali ya kupunguza hatari ya kutokea kwa majanga.

Akizungumza pambizoni mwa kongamano la 8 la kanda ya Afrika kuhusiana na mbinu za kupunguza majanga- Disaster Risk Reduction lililoandaliwa jijini Nairobi, Munde alisema taifa la Malawi lilijumuisha watu wenye ulemavu katika miradi kwani waligundua kuwa watu hao huathirika sana.

‘Watu wenye ulemavu huathirika kwa njia tofauti majanga yanapotokea, kwahivyo ni bora watu wenye ulemavu wajumuishwe kwani hao ndio wanajua shida wanazopitia’, Alisema Munde.

Usemi ulioungwa mkono na Olivia Chibgwe afisaa mkuu wa utawala kutoka Zimbabwe, ambaye alisema kuna haja kuwajumuisha watu wenye ulemavu endapo mataifa yanataka matokeo bora kuhusu jinsi ya kupunguza hatari ya kutokea kwa majanga.


 

More Stories

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo