Bei ya mafuta imepanda na kuvuka dola mia moja kwa mara ya kwanza tangu miaka saba iliyopita.

Ongezeko hilo limesababishwa na hofu juu ya ugavi baada ya mzalishaji mkubwa Urusi kufanya mashambulio nchini Ukraine.

Bei ya mafuta ghafi barani Ulaya imefikia dola 105 na senti 79 kwa pipa.

Mnamo mwaka 2020 bei ya bidhaa hiyo ilianguka kutokana na athari ya maambikizi ya virusi vya corona.

Urusi ni mzalishaji muhimu wa mafuta baada ya Saudi Arabia miongoni mwa nchi za shirika la wauzaji mafuta la OPEC.