Zaidi ya wanahabari wakike 180 kutoka mataifa 10 barani Afrika wamejiunga katika mpango wa mafunzo wa Win Leadership Accelerator kupitia shirika la Women in News Accelerator program.

Mmoja mwa wanahabari wetu Nuru Mwalimu ni miongoni mwa waliofaulu katika kitengo hicho.

Mpango huo utakaochukua muda wa miezi 9 unalenga kuwajenga wanahabari na wahariri wakike kitaaluma na ujuzi wa kuongoza na kuimarisha vyumba vya habari barani Afrika.

Aidha mafunzo hayo yanalenga kuimarisha wanahabari wakike katika kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo katika taaluma ya uanahabari.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo kupitia njia ya mtanadao mkurugenzi wa shirika la Win Africa Jane Godia amesema idadi ya washirika mwaka huu umeongezeka mara dufu ikilinganisha na Miaka ya nyuma huku idadi kubwa ya washirika waliotangulia wakifaulu.

Miongoni mwa mataifa yalioshiriki barani ni pamoja na Kenya, Uganda, Somali, south Sudan Tanzania Malawi.