Bei ya mafuta imeongezwa kwa Ksh9.90 katika tathmini ya mwezi Aprili ya Mamlaka ya Uthibiti wa Kawi (EPRA).

Hii inaaminisha lita moja ya petroli jijini Nairobi imepanda kutoka Ksh114.62 hadi Sh134.72.

Lita moja ya dizeli sasa itauzwa Ksh 125.50 kutoka Sh115.60.

Mafuta taa itauzwa shilingi 113. 44 jijini Nairobi kutoka Sh 103.54.Bei mpya zitaanza kutumika saa sita usiku wa Alhamisi, Aprili 14 hadi saa sita usiku wa Mei 14, 2022.

Afisa Mkuu Mtendaji wa EPRA Daniel Kiptoo amesema bei hizo mpya zinajumuisha asilimia 8 ya VAT kwa mujibu wa Sheria ya Fedha, 2018, Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushuru ya 2020 na marekebisho ya viwango vya mfumuko wa bei.