Miamba ya matumbawe ni mawe laini yanayopatikana chini ya bahari au kando mwa bahari na hivyo basi kufahamika kama msitu wa baharini.

Lakini ongezeko la joto na kiwango cha maji ya bahari kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kumeharibu mazingira ya baharini.

Mhariri wetu Ruth Keah alipata fursa ya kutembelea kituo cha Reefolution kinachojihusisha na uhifadhi na upanzi wa miamba ya matumbawe baharini katika eneo la Mkwiro katika kisiwa cha Wasini kaunti ya Kwale.

Ambapo alikutana na Cindy Saru Chorongo, Msichana wa miaka 23 anayepiga mbizi baharini na kupanda matumbawe na kufanya mahojiano naye.