Huku gharama ya maisha ikizidi kuongezeka serikali imeshauriwa kuweka mazingira bora ya kufanya biashara nchini ili wafanyabiashara waweze kufanya biashara kwa urahisi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa tawi la Naivas Bombolulu hapa Mombasa mkurugenzi mkuu wa mauzo katika maduka hayo Willy Kimani amesema kuna haja ya serikali kuwacha kupiga siasa na kuhakikisha kuwa mazingira ya biashara nchini yanaboreshwa.

Aidha amesema kuwa hali ilioko kwa sasa imechangia kupungua kwa biashara hasa ikizingatiwa kuwa wateja wanalazimika kupunguza mahitaji yao kutokana na ugumu wa maisha..

Kufunguliwa kwa tawi hilo jipya kumefikisha idadi jumla ya maduka ya Naivas nchini kufikia 94 ambapo kulingana na mkurugenzi huyo zaidi ya vijana elfu 10 wameweza kupata ajira huku maduka 6 zaidi yakitarajiwa kufunguliwa katika sehemu mbalimbali za nchi mwaka huu ili kufikisha idadi jumla ya maduka 100.