Waziri wa madini na uchumi samawati Salim Mvurya amesema kuwa serikali inapanga kufanya uvuvi kuwa mojawapo ya sekta za uwekezaji.
Akizungumza katika hafla iliyoandaliwa katika taasisi ya uvuvi na utafiti wa baharini KMFRI, Mvurya amesema muda umewadia kwa wavuvi kujisajili kama vyama vya ushirika ili kufaidika na miradi iliyowekwa na serikali katika sekta ya uvuvi.
Waziri huyo amesema kuwa serikali imetoa shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya mpango huo.
Vile vile Mvurya amesema serikali inalenga kuimairisha miundo msingi katika maeneo yaliyo na bahari au mito ili kuimarisha sekta ya uvuvi
Aidha amewataka viongozi katika sekta ya uchumi samawati kujukumika katika majukumu waliyopewa.

Wakulima katika kaunti ya Lamu wamehimizwa kutumia maghala yaliyojengwa na serikali kwa ajili ya kuhifadhi mazao yao.
Gavana wa kaunti ya Lamu Issa Timamy amesema kaunti hiyo iko na maghala manne ambayo yalijengwa kwa ajili ya wakulima na hakuna anayetumia maghala hayo.
Amesema kutokana na mvua inyavyoendelea kunyesha kuna matumaini ya watu kupata mavuno mazuri mwaka huu hivyo basi mazao hayo yanapaswa kuhifadhiwa vyema kabla ya kuuzwa.
Timamy ametoa wito kwa wakulima kuhifadhi mazao yao katika maghala ya serikali ili kuepuka hasara ya mazao hayo kuharibika au kununuliwa kwa bei duni kwani baadhi ya wafanyibiashara huwanyanyasa wakulima kwa kuwanunulia mazazo yao kwa bei ya chini sana.
Aidha amesema bajeti ya kilimo ya mwaka ujao itaongezwa ili kuboresha zaidi kilimo katika kaunti hiyo na kuongeza kiwango cha uzalishaji wa chakula kwa ajili ya wakaazi wa Lamu na hata kwa ajili ya biashara.


Huku gharama ya maisha ikizidi kuongezeka serikali imeshauriwa kuweka mazingira bora ya kufanya biashara nchini ili wafanyabiashara waweze kufanya biashara kwa urahisi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa tawi la Naivas Bombolulu hapa Mombasa mkurugenzi mkuu wa mauzo katika maduka hayo Willy Kimani amesema kuna haja ya serikali kuwacha kupiga siasa na kuhakikisha kuwa mazingira ya biashara nchini yanaboreshwa.

Aidha amesema kuwa hali ilioko kwa sasa imechangia kupungua kwa biashara hasa ikizingatiwa kuwa wateja wanalazimika kupunguza mahitaji yao kutokana na ugumu wa maisha..

Kufunguliwa kwa tawi hilo jipya kumefikisha idadi jumla ya maduka ya Naivas nchini kufikia 94 ambapo kulingana na mkurugenzi huyo zaidi ya vijana elfu 10 wameweza kupata ajira huku maduka 6 zaidi yakitarajiwa kufunguliwa katika sehemu mbalimbali za nchi mwaka huu ili kufikisha idadi jumla ya maduka 100.

Show more post

 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo