Picha Kwa Hisani ya Thomas Bwire

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya watu wenye ulemavu,jamii ya watu wenye ulemavu wamekanusha madai kuwa wao wanaongoza katika shughuli za omba omba mijini.

Fred Ouko ambaye ni afisa wa mipango kutoka kwa shirika la watu wenye ulemavu la Open Society Initiative for Eastern Africa,amekanusha madai kuwa jamii ya watu wenye ulemavu wanajihusisha na shughuli za omba omba mijini.

Ouko ametaja kuwa wengi wanao omba omba mijini sio walemavu bali ni matapeli wanaojifanya kuwa walemavu,hivyo kuwasihi wanahabari kutowahusisha watu wenye ulemavu na shughuli za watu  omba omba mijini.

Picha kwa hissani ya Thomas Bwire

Wakati huo huo jamii imetakiwa kutowatenga na kuondoa dhana potofu kuwa watu wenye ulemavu wamelaaniwa katika jamii.

Kulingana na afisa wa mipango na miradi katika shirika la kimataifa la Internews Jackline Lidubwi, watu wenye ulemavu wana haki kama watu wengine na kamwe hawajalaaniwa kama inavyo dhananiwa.

Ameisihi jamii kushirikiana na watu wenye ulemavu katika maswala yote ya jamii na kiuchumi kwani wana uwezo wa kutekeleza majuku mbali mbali kama watu wengine.

Lidubwi amewasihi wanahabari kutumia maneno yanayostahili wanapoangazia habari za watu wenye ulemavu ili jamii iwe kuwatambua watu hao.Aidha amesisitiza haja ya kuajiriwa kwa wanahabari wenye ulemavu ambao watakuwa kipaumbele katika kuangazia masilahi ya watu wenye ulemavu.

Lidubwi ameyasema haya pambezoni mwa kongamano la kuwafunza wanahabari namna ya kuangazia habari za watu wenye ulemavu jijini Nairobi.


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo