Nigeria kuminyana na Ivory Coast katika fainali ya AFCON huku Afrika kusini wakisaka nafasi ya tatu dhidi ya Jamhuri ya kidemokrasia Congo.

Mtanange wa kumtafuta mshindi wa tatu wa AFCON kati ya Afrika Kusini na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo itapigwa jumamosi saa tano usiku huku fainali ikigaragzwa jumapili kati ya wenyeji Ivory Coast na Nigeria.

Wenyeji Ivory coast mara ya mwisho kushinda kombe la AFCON ilikua mwaka 2015 wakiongozwa na nahodha Yaya Toure huku wapinzani wao Nigeria walishinda taji hilo la AFCON 2013.

Nigeria walitingia fainali baada ya kushinda mechi yao ya nusu fainali dhidi ya Afrika kusini kupitia mikwaju ya penalti, nao Ivory coast waliipiga Congo goli moja bila jawabu lililofungwa na mchezaji Sebastian Haller.

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Sebastien Desabre amesema anatumai timu yake itatumia mechi hii ya nusu-fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON ili "kuwafariji" raia wa Kongo.

Sebastien Desabre amesema anatarajia kuwa timu itawapa burudani la soka wakongo wanaoteseka kutokana na ghasia zinazoendelea mashariki mwa taifa hilo.

Desabre amewaambia waandishi wa habari mjini Abidjan kwamba mechi ya leo dhidi ya wenyeji Ivory Coast ni maalum, na wanataka watu wanaoteseka huko Kongo wajivunie timu yao ya taifa na kwamba ni kazi yao kuwapa watu furaha na kuwafanya watabasamu.

DRC itatumia ngarambe hiyo ya Nusu fainali kutuma ujumbe na kutoa pole kwa waathiriwa wa mapigano Kaskazini mwa nchi hiyo.

DRC Wamesema kuwa hawatavaa jezi kwa ajili ya kupata ushindi bali kutuma ujumbe lakini pia na kutoa pole kwa wahanga wa mapigano lakini pia na kuomba maridhiano kati ya Serikali na Waasi.

Nahodha wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Chancel Mbemba amechapisha ujumbe unaosema kuwa “Naomba mara kwa mara nchi yangu iweze kurejea katika hali ya utulivu na watu wapate amani”.

Kocha wa DRC ambaye ni raia wa Ufaransa amefanya mabadiliko makubwa katika timu hiyo tangu alipochukua mikoba mwezi Agosti mwaka 2022 baada ya Kongo kupoteza mechi zao mbili za mwanzo za kuwania kufuzu kwenye michuano hiyo.

Katika mechi za leo Jumatano (07.02.2024) za nusu fainali ya michuano ya AFCON, timu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo itachuana na Ivory Coast huku Nigeria ikishuka dimbani na Afrika Kusini.

Nigeria ambayo mchezaji wake nyota Victor Osimhen atakuwa uwanjani leo baada ya kuwepo hofu kwamba huenda angeukosa mchezo huo muhimu kutokana na jeraha.

Licha ya wachambuzi wengi wa soka kusema kuwa Nigeria na wenyeji Ivory Coast wana nafasi kubwa ya kushinda mechi za leo, dakika 90 ndizo zitakazoamua timu gani zitakazotoana kijasho kwenye fainali ya AFCON.

 

Nyota ya Mlinda lango Chuma Mohammed inaendelea kung’aa baada ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa Harambee stars chini ya umri wa miaka 20.

Mwaka 2023 umekua mzuri kwa Chuma baada ya kutwaa tuzo ya kipa bora pamoja na kusaidia timu yake ya Mombasa Maize Millers kuwa mabingwa wa Taifa Ngano Super cup mnamo oktoba 29 katika uwanja wa Mombasa sports club .

Kipa huyo mahiri pia alitamba katika michuano inayoendelea ya Rashid Abdallah super cup Makala ya nne akiichezea Kundutsi FC iliyobanduliwa na Wailers katika hatua ya robo fainali.

Chuma ameiwakilisha kaunti yay a Mombasa kwenye michuano ya talanta hela kwa wachezaji wasizidi umri wa miaka 19.

Kwenye michuano hiyo ya Talanta hela kanuti ya Mombasa ilitolewa na kaunti ya homa baya kwenye hatua ya robo fainali.

Homa bay ndio mabingwa wa talanta hela baada ya kuichapa Kisumu mabao 4-2 kwenye fainali iliyopigwa katika maadhimisho ya 60 tangu kupata uhuru siku ya jumanne katika uwanja wa nyayo.

Kwenye michuano hiyo ya Talanta hala Chuma aliandikisha cleansheet nyingi kuliko kipa kipa yeyote .

Rahma Viwanjani inamtakia kila la heri kipa Chuma Mohamed.

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la soka nchini Cameroon, imetupilia mbali barua ya kujiuzulu ya Rais wa Shirikisho hilo Samuel Eto’o.

Ombi la Samuel Eto’o kujiuzulu kama Rais wa FECAFOOT limekataliwa na kamati Utendaji bila kujali mwenendo mbaya wa timu ya Taifa ya Cameroon nchini Ivory Coast kwenye michuano ya AFCON.

Kamati hiyo bado inaamini kuwa Eto’o anasalia kuwa mtu sahihi kuongoza Shirikisho hilo.

Samuel Eto’o anashutumiwa katika upangaji wa matokeo na vitisho kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Cameroon.

 

Baada ya Denmark,Azzam, Kwale United , Kombani Youth,Mshale, Kitivo, Dumna na Kundutsi kutinga raundi ya 16 bora kwenye mechi zao za wikendi iliyopita kwenye ligi ya Rashid Abdalla Super Cup, wikendi hii kutagaragzwa mechi nyengine nane za kutamatisha hatua ya makundi kwenye ligi hiyo.

Na siku ya Jumamosi saa tisa na nusu kutapigwa mechi nne katika viwanja mbalimbali huko Kwale.

Uwanjani Waa Black Eagles watamenyana na Lazium fc.

Kwale Teachers wakabane koo na Wayzata Boys FC katika uwanja wa Kombani .

Marika FC watoane kijasho na Rsing Stars katika uga wa Mkokoni.

Katika uga wa Denmark hapo maganyakulo Lutembe watavaana na Vivah Manyota FC.

Siku ya Jumapili itakua zamu ya Albion Youth kumenyana na Desert FC kwenye uwanja wa Mkokoni.

Fafada Fc watakua katika uchanjaa wa Waa kubwagana na Bongwe United.

Wailers FC watakipiga dhidi ya FC Talibase uwanjani Denmark Maganyakulo.

Katika uga wa Kombani Morocco watamenyana na Green Boys FC .

Mechi zote za jumapili zitaanz asa atisa na nusu.

 

 

Show more post

 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo