Baraza la kitaifa la makanisa nchini (NCCK) linawataka viongozi wa kisiasa watakaoshindwa kwenye kura kukubaliana na matokeo ya uchaguzi.

Mwenyekiti wa baraza hilo katika eneo la pwani askofu Peter Mwero amewaonya wanasiasa dhidi ya kuvuruga amani endapo watapinga matokeo ya kura.

Mwero amewataka wagombea wa nyadhfa tofauti za kisiasa wataokosa kukubaliana na uamuzi wa wananchi kuelekea mahakamani ili kutafuta haki.

Ni kauli iliyoungwa mkono na afisa tawala wa polisi kaunti hiyo mchungaji Patrick Irina aliyesema kuwa hatua hiyo itawazuia vijana dhidi ya kutumiwa vibaya na wanasiasa kuzua vurugu.

Aidha Irina amesema kuwa idara ya usalama kaunti hiyo inalenga kutoa ushauri nasaha kwa viongozi watakaokumbwa na msongo wa mawazo baada ya kushindwa kwenye uchaguzi.