Serikali ya kaunti Mombasa inalenga kufanya zoezi la matibu ya bure katika Wadi 30 zilizopo katika kaunti ya Mombasa kuanzia mwezi huu wa Mei.

Kulingana na gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir zoezi hilo litawezesha kusajili familia elfu 10 kila Wadi katika mpango wa kadi ya bima ya afya NHIF.

Nassir hata hivyo amewapatia majukumu wahudumu wa afya wa kujitolea CHVs kutambua wale wanaostahili kupewa bima ya afya pindi tu zoezi hilo litakapo noa nanga rasmi.