Mawakili wanaosimamia kanisa la New life linalomilikiwa na pasta Ezekiel Odero wametofautiana vikali na jopo lililoundwa na rais la kutathmini mwongozo wa dini hapa nchini.

Mawakili Cliff Ombeta na Danstan Omar wamesema jopo hilo halijawapa wakati mzuri viongozi wa kidini kutoa maoni yao.

Wakizungumza mjini Kilifi wakati wa kutoa maoni kwa jopo hilo,mawakili hao wamemlaumu mwenyekiti wa jopo hilo Mutava Musyini kwa kutowajibikia majukumu yao.

Kwa upande wake Mutava amepinga malalamishi hayo na kusema kuwa kila mkenya amepewa nafasi sawa kutoa maoni yake.